JINSI YA KUTENGENEZA ICE CREAM LAINI NA TAMU SANA

 JINSI YA KUTENGENEZA ICE CREAM LAINI NA TAMU SANA

MAHITAJI

1.      Unga wa ubuyu 1/2

2.      Sukari 3/4

3.      Unga wa muhogo vijiko viwili (2) vya chai

4.      Rangi aina yoyote uipendayo ya chakula

5.    Maji lita 5

6.     Radha

7.     Mifuko ya kufungia
 


HATUA

1.    Weka unga wa ubuyu kwenye sufuria lako la kuchemshia pamoja na unga wa muhogo hii husaidia Ice Cream zetu ziwe laini, wengine hutumia Coin Flower.

2.    Acha ubuyu uchemke huku ukiukoronga koronga mpaka uwe mzito.

3.    Ubuyu unatakiwa upoe kwa dakika 5.

4.    Uchuje ubuyu 

5.    Ukiwa tayari unatakiwa uchanganye sukari, rangi pamoja na radha uipendayo kama vile Straberry, Orange, Pinepple n.k.

6.    Ice Cream zetu zitakuwa ziko tayari kwa kufunga na kuwekwa kwenye Friji kwa ajili ya kuuza.




Comments